Rais Putin ameviweka vikosi vya nyuklia vya Urusi katika tahadhari "maalum", na kuzua wasiwasi kote ulimwenguni.
Lakini wadadisi wa mambo wanadokeza kwamba hatua zake huenda zikatafsiriwa kuwa onyo kwa nchi nyingine kutozidisha ushiriki wao nchini Ukraine, badala ya kuashiria kutaka kutumia silaha za nyuklia.
Silaha za nyuklia zimekuwepo kwa takriban miaka 80 na nchi nyingi zinaziona kama kizuizi kinachoendelea kudhamini usalama wa taifa lao.
Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
Takwimu zote za silaha za nyuklia ni makadirio lakini, kwa mujibu wa Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, Urusi ina vichwa vya nyuklia 5,977 - vifaa vinavyosababisha mlipuko wa nyuklia - ingawa hii inajumuisha takriban 1,500 ambazo zimechoka na zinatazamiwa kuvunjwa.
Kati ya 4,500 zilizosalia au zaidi, nyingi zinachukuliwa kuwa silaha za kimkakati za nyuklia - makombora ya balestiki, au makombora, ambayo yanaweza kulengwa kwa umbali mrefu. Hizi ndizo silaha ambazo kawaida huhusishwa na vita vya nyuklia.
Zilizosalia ni silaha ndogo za nyuklia zisizoweza kuharibu sana kwa matumizi ya masafa mafupi kwenye uwanja wa vita au baharini.
Lakini hii haimaanishi kuwa Urusi ina maelfu ya silaha za nyuklia za masafa marefu tayari kwenda.
Wataalamu wanakadiria takribani vichwa 1,500 vya kivita vya Urusi kwa sasa "vimetumwa", kumaanisha kuwa viko kwenye kambi za makombora na mabomu au kwenye manowari baharini.
Je, hii inalinganishwaje na nchi nyingine?
Nchi tisa zina silaha za nyuklia: China, Ufaransa, India, Israel, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Marekani na Uingereza.
China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza pia ni miongoni mwa mataifa 191 yaliyosaini Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
Chini ya makubaliano hayo, wanapaswa kupunguza akiba yao ya silaha za nyuklia na, kwa nadharia, wamejitolea kutokomeza kabisa.
Na imepunguza idadi ya vichwa vya kivita vilivyohifadhiwa katika nchi hizo tangu miaka ya 1970 na 80.
India, Israel na Pakistan hazikuwahi kujiunga na NPT - na Korea Kaskazini iliondoka mwaka 2003.
Israel ni nchi pekee kati ya tisa ambayo haijawahi kukiri rasmi mpango wake wa nyuklia - lakini inakubaliwa na wengi kuwa na vichwa vya nyuklia.
Ukraine haina silaha za nyuklia na, licha ya shutuma za Rais Putin, hakuna ushahidi kuwa imejaribu kuzipata.
Silaha za nyuklia zina uharibifu gani?
Silaha za nyuklia zimeundwa kusababisha uharibifu mkubwa zaidi.
Kiwango cha uharibifu hutegemea mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
• Ukubwa wa kichwa cha silaha
• Jinsi inavyolipua juu ya ardhi
• Mazingira ya ndani