Subscribe Us

Header Ads

Simba Yapata Balaa Jingine, Kiongozi Afrika Kusini Aishitaki CAF Kisa Moto Uwanjani




Klabu ya Simba iliwasha moto uwanjani kwenye pambano lao dhidi ya Klabu ya Orlando Pirates
MTENDAJI MKUU wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiuanamichezo.

Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuona hatua stahiki zinachukuliwa.


Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe
Klabu ya Simba ilitolewa na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya hatua hiyo ya mtoano.