Subscribe Us

Header Ads

Polisi Indonesia yatumia gesi ya kutoa machozi kuzima maandamano



Polisi ya Indonesia imetumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kutawanya mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa wakiandamana kupinga ongezeko la bei ya mafuta na kuongezwa muda wa kukaa madarakani kwa Rais Joko Widodo. 

Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters, idadi kubwa ya waandamanaji walionekana kukimbia kutoka maeneo ya bunge katika mji mkuu Jakarta, huku runinga ya Kompas ikisema mawe yalirushwa nje ya majengo ya bunge. 

Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika miji mbalimbali ya Indonesia leo Jumatatu ikiwemo Sulawesi Kusini, Magharibi mwa Java na Jakarta. 

Tangu jadi, wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa nguzo muhimu katika juhudi za kulinda mafanikio ya kidemokrasia ya nchi hiyo, baada ya kufanya maandamano makubwa mnamo mwaka 1998 yaliyosaidia kumuondoa madarakani rais wakati huyo, Haji Suharto.