Subscribe Us

Header Ads

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa aanza ziara Yemen

 


Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen, Hans Grundberg, ameanza ziara yake ya kwanza katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Sanaa kufuatia makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mnamo Aprili 2, japo pande zinazohasimiana zimekuwa zikilaumiana kwa ukiukaji wa makubaliano hayo ya kusitisha vita. 

Mwanadiplomasia huyo wa Uswidi anatarajiwa kukutana na maafisa wa kundi la Huthi katika ziara hiyo ya Sanaa kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi Septemba. 

Ofisi ya Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa imeandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa, Grundberg atafanya mazungumzo na uongozi wa Huthi juu ya kutekeleza na kuimarisha makubaliano hayo ya amani na kujadili pia juu ya mkondo wa baadaye. 

Usitishaji wa vita wa miezi miwili ulitangazwa mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, na kwa kiasi kikubwa umetekelezwa.