Rais Mteule wa Korea Kusini Yoon Suk-Yeol's amesema serikali yake itatoa fidia ya dola bilioni 42 kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wameathiriwa na vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona.
Taarifa ya ofisi ya kiongozi huyo ambae anatarajiwa kuanza kazi rasmi Mei 10 imesema malipo hayo yatazingatia waathirika katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021.
Hata hivyo taarifa hiyo ya ofisi ya rais mteule haijasema kiasi gani hasa kitakacholipwa au kutaja ukubwa wa bajeti ya ziada inayotarajiwa.
