Wabunge wa Somalia leo hii wamemchagua Sheikh Adan Mohamed Nur kuwa spika wao mpya leo, katika uchaguzi uliocholeweshwa kutokana na kutokubaliana juu ya nani atakuwa kiongozi wa usimamizi wa usalama wa eneo la kupigia kura.
Nur aliibuka na ushindi katika uchaguzi uliosimamiwa na spika wa mpito Abdisalan Liban Dhabancad.
Kuchelewa kwa uchaguzi nchini Somalia kumetokana na vurugu za makundi ya wafuasi wa itikakadi kali na mzozo wa madaraka kati ya rais Mohamed Abdullahi Mohamed na waziri mkuu Mohamed Hussein Roble.
Mahasimu hao wa siasa za Somalia, wote wamempogeza spika mpya kupitia kurasa zao za Twitter.
Uchaguzi huu wa spika katika bunge na seneti ni hatua muhimu katika kukamilisha mchakato wa kuundwa kwa serikali mpya, ambayo lazima iwe tayari kufikia Mei 17 endapo Somalia itataka kuendelea kupokea msaada wa bajeti kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.
