Rais Volodomyr Zelensky leo hii amesema amezunguzumza kwa njia ya simu na mwenziwe wa Marekani, Joe Biden na kujadili msaada wa kifedha pamoja na vikwazo dhidi ya Urusi katika kipindi hiki ambacho taifa lake likikabiliwa na ongezeko la mashambilizi.
Katika ukurasa wake wa Twetter, Zelensky kama sehemu ya nazungumzo yake ya mara kwa mara amefanya tena mazungumzo na Biden, na ajenda zilikuwa masuala ya usalama, msaada wa kifedha na kuendelezwa kwa vikwazo dhidi ya Urusi.
Masaa kadhaa awali, kiongozi huyo wa Ukraine alikuwa amewahutubia wabunge wa Marekani kupitia njia ya video, akiomba msaada zaidi kwa nchi yake iliyozingirwa na kugoma pia uagizaji wa mafuta kutoka Urusi.
Wabunge wa Marekani waliahidi msaada wa ziada wa kitita cha dola bilioni 10, lakini Ikulu ya Marekani White House imeondoa marufuku ya mafuta, ikihofia ongezeko la bei na kuwaumiza watumiaji wa Marekani ambao tayari wameathirika na mfumuko wa bei.