Subscribe Us

Header Ads

Watu 21 wauawa katika mji wa Sumy Ukraine wakati maeneo ya kiutu yakifunguliwa

 



Zaidi ya watu 21 wakiwemo watoto wawili wameuawa katika mashambulizi ya kutokea angani kwenye mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine, Sumy. 


Mashambulizi hayo yalifanywa saa chache tu baada ya kufunguliwa kwa maeneo salama ya kiutu kwa ajili ya raia kukimbia mapigano. Mkuu wa serikali ya mkoa wa Sumy amesema katika baadhi ya maeneo nyumba za makazi zililipuliwa kwa mabomu. 


Haikuwezekana kuthibitisha taarifa hizo kwa njia huru. Jeshi la Urusi lilianza kutekeleza mpango wa usitishwaji mapigano leo na kufungua maeneo ya kiutu katika miji mitano ambayo ni Kyiv, Chernihiv, Kharkiv, Sumy na mji wa bandari wa Mariupol. 


Wakaazi wa Sumy walihamishwa kwenye mabasi na magari madogo hadi mji wa katikati ya Ukraine Poltava.