Subscribe Us

Header Ads

Wanajeshi wa 27 wa Mali wauawa katika shambulizi


 


Wanamgambo wa itikadi kali wamevamia kambi ya kijeshi katika eneo la katikati mwa Mali hapo jana na kuwauwa takriban wanajeshi 27 na kuwajeruhi vibaya wengine 24 katika shambulizi baya zaidi mwaka huu. 

Haya yameripotiwa na shirikia la habari la serikali ORTM.Shirika hilo limeendelea kuripoti kuwa shambulizi hilo lilitokea karibu na mji wa Mondoro ulio karibu na mpaka unaokabiliwa na ghasia kati ya Mali na Burkina Faso. 

Shambulizi hilo la jana limejiri wakati kuna ongezeko la hofu kwamba wanamgambo wa itikadi kali huenda wakashika udhibiti wakati vikosi vya Ufaransa vikijiandaa kuondoka nchini humo katika miezi ijayo. 

Mwezi uliopita, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuwa kuondolewa kwa vikosi vya nchi yake kutafanyika katika muda wa miezi sita ijapokuwa mamlaka nchini Mali imesema kuwa Ufaransa inapaswa kufanya hivyo bila kuchelewa.