Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, linawashikilia wanafunzi sita wa shule ya sekondari Mwenge iliyopo mjini Singida, kwa tuhuma za kuchoma moto pikipiki ya mwalimu yenye namba za usajili MC 653 BFS pamoja na kufyeka shamba la mahindi lenye ukubwa wa ekari moja.
Hii ni baada ya mwalimu huyo kumchapa mwanafunzi mwenzao aliyeficha simu darasani.