Subscribe Us

Header Ads

Vikosi vya Ukraine vinadai kutwaa tena Chuhuiv



 Maafisa wa ulinzi wa Ukraine wanadai kuwa vikosi vyao vimeuteka tena mji wa mashariki wa Chuhuiv.


Katika taarifa kuhusu operesheni iliyotumwa kwenye Facebook Jumapili usiku, Mkuu wa jeshi la Ukraine alisema kwamba vikosi vya Kyiv viliuteka mji huo kutoka kwa wanajeshi wa Urusi na kuvisababishia hasara kubwa vikosi vya Moscow wakati wa vita.


Maafisa wa Ukraine pia walidai kuwa makamanda wawili wa ngazi za juu wa Urusi waliuawa wakati wa vita vya kuwania mji huo, ambao una idadi ya watu wapatao 31,000.


BBC haiwezi kuthibitisha madai haya kwa uhuru.


Chuhuiv iko katika eneo la kimkakati karibu maili 23 kutoka mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine Kharkiv, ambao umekuwa chini ya mashambulizi ya makombora makubwa kutoka kwa vikosi vya Urusi kwa zaidi ya wiki