Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg anasema kuna ushahidi kwamba Urusi inatumia mabomu ya mtawanyiko (cluster) katika uvamizi wake.
Katika mkutano na waandishi wa habari, aliwaambia waandishi wa habari: "Tumeona matumizi ya mabomu ya mtawanyiko na tumeona ripoti za matumizi ya aina nyingine za silaha ambazo zitakuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Pia anasema muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi hautaweka marufuku ya kuruka ndege juu ya anga ya Ukraine wala kutuma wanajeshi wake huko lakini anaahidi msaada mwingine kwa Kyiv na kumtaka Rais Vladimir Putin kukomesha uvamizi huo mara moja.