Mashambulizi ya Urusi katika maeneo yenye watu wengi nchini Ukraine ni juhudi za kuvunja ari, kulingana na wizara ya ulinzi ya Uingereza.
Katika ripoti yake ya kila siku ya kijasusi, MoD inasema nguvu ya upinzani wa Ukraine inaendelea kushangaza Urusi, ambayo imejibu kwa kulenga miji ikiwa ni pamoja na Kharkiv, Chernihiv na Mariupol.
Inalinganisha mkakati wa Urusi na kampeni zake nchini Syria mwaka wa 2016 na Chechnya mwaka 1999, wakati jeshi la Urusi lilipofanya mashambulizi makali ya maeneo yaliyojengwa.
Ripoti hiyo pia inasema kwamba maendeleo ya Urusi yamepunguzwa na Ukraine kulenga laini zake za usambazaji.
Inalinganisha mkakati wa Urusi na kampeni zake nchini Syria mwaka wa 2016 na Chechnya mwaka 1999, wakati jeshi la Urusi lilipofanya mashambulizi makali ya maeneo yaliyojengwa.Ripoti hiyo pia inasema kwamba maendeleo ya Urusi yamepunguzwa na Ukraine kulenga laini zake za usambazaji.