Subscribe Us

Header Ads

Ruto aidhinishwa kugombea urais wa Kenya


 


Zaidi ya wajumbe 5000 wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) wamemuidhinisha Naibu wa Rais wa Kenya William Ruto kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.


Kufuatia uidhinishaji wake rasmi, naibu Ruto atachuana na mgombeaji wa wa Muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga miongoni mwa wagombea wengine.


Bw. Ruto alikubali ridhaa hiyo mbele ya mawakili wa chama hicho na kuapa kuilinda Katiba ya Chama cha UDA katika kinyang’anyiro cha urais.


"Mimi, William Ruto, nakubali kwa dhati kuwa mgombea urais wa chama cha United Democratic Alliance katika uchaguzi Mkuu wa Kitaifa utakaofanyika Agosti 2022," Ruto aliapa mbele ya wajumbe.


"Nitatumikia wanachama wa chama kwa bidii kulingana na mwenendo wa uchaguzi wa chama na kuwatumikia wanachama wa chama kwa bidii kama mgombeaji wa urais," aliongeza.


Rais Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9, mwaka huu.