Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni alikutana na balozi wa Urusi Vladlen Semivolos siku ya Alhamisi kujadili "masuala yenye maslahi kwa pande zote mbili".
Hakutoa maelezo zaidi, lakini ilikuja siku moja baada ya Uganda kujizuia kupiga kura kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Nchi nyingine 16 za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Angola, Algeria na Mali hazikupiga kura.
Mtoto wa kiume wa Rais Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jumatatu alieleza kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika ujumbe