Subscribe Us

Header Ads

Rais Samia azindua jengo la Makao Makuu CRDB




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Machi 5, 2022 amezindua Jengo la Makao Makuu ya Benki ya CRDB lililopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Posta jijini Dar es Salaam.


Katika hafla hiyo Rais Samia amewataka watendaji wa CRDB kulitunza jengo hilo pia kulitumia kama chachu ya kufanya vizuri zaidi kwasababu jengo ni la kisasa.

"Niwatie moyo CRDB nendeni kokote kule mnapoona mnaweza kuwekeza nendeni, kwa kuwa hata mabenki ya nje yanakuja huku nchini, mwanangu Juma Nature aliwahi kuomba, kwani wao wanaweza wana nini hata sisi tushindwe tuna nini" - Rais Samia Suluhu.