Subscribe Us

Header Ads

Mradi wa maji wa Sh41.5 bilioni wazinduliwa Simanjiro

 


 


Makamu wa Rais Dk Philip Mpango leo Jumanne Machi 15, 2022 ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet unaogharimu Sh41.5 bilioni uliopo Simanjiro mkoani Manyara.


Dk Mpango amezindua mradi huo uliofadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania ambao umekamilika kwa asilimia 99.


Akizungumza na wananchi wa Loiborsoit mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo, Makamu wa Rais amewata wananchi wa eneo hilo kuendelea kulinda mazingira ili kutopoteza chanzo cha maji kilichopo katika eneo hilo kinachotegemewa katika mradi mkubwa wa maji wa Orkesumet.


"Mradi huu utawanufaisha wananchi na kuwapunguzia mzigo wanawake waliokuwa wanatumia saa tano kufuata maji kwa punda," amesema Dk Mpango.


Kwa upande wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema wizara itaendelea kutekeleza miradi kwa ufanisi pamoja na kuokoa gharama zisizo za lazima katika utekelezaji wa miradi hiyo.


Waziri aweso amesema utakelezwaji wa mradi huo kwa kutumia wakandarasi wa ndani unatoa fursa ya kuaminiwa kwa wakandarasi wa ndani ya nchi huku akiwataka watendaji katika wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita.