Subscribe Us

Header Ads

Mlipuko wa bomu wauwa zaidi ya 30 na kujeruhi 56 Pakistan



Polisi nchini Pakistan imesema zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa, kufuatia mlipuko mkubwa katika msikiti wa Kishia kwenye mji wa Peshwar, ulioko kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

 Afisa wa polisi mjini humo, Waheed Khan, amesema mlipuko huo ulitokea wakati waumini wakiwa wamekusanyika katika msikiti wa Kucha Risaldar katika mji mkongwe wa Peshwar kwa ajili ya sala ya Ijumaa. 

Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na shambulio hilo, lakini makundi ya Dola la Kiislamu na kundi la Taliban la Pakistan yamefanya mashambulizi kama hayo kwenye eneo hilo, lililoko karibu na mpaka na Afghanistan. Waziri Mkuu Imran Khan amelaani shambulio hilo.