Kuku ni ndege wafugwao na binadamu wengi kwa ajili ya matumizi mbalaimbali ya binadamu. Mara nyingi hutumika kwa ajili ya kitoweo na kwa biashara pia. wafugaji wengi hupenda kufuga kuku maana ni mwepesi kumtunza na hana garama kubwa za utunzaji ukilinganisha na wanyama wengine wafugwao.
Leo tutaangalia jinsi ya kuwalea vifaranga hadi wafae kuwa kuku wakubwa;
Nyumba ya vifaranga
Nyumba ya vifaranga inatakiwa kuwa karibu na nyumba ya kuishi ili uweze kuwaangalia vifaranga kwa ukaribu zaidi, ijengwe kwenye sehemu iliyotulia kulingana na mwelekeo wa upepo na kuta zisiingize baridi sana pia iwe na eneo la kutosha kulelea vifaranga.
Baadhi ya wafugaji hutengeneza nyumba za kufugia ilimradi katengeneza bila kutumia vipimo au ufanisi mzuri ili kulea vifanganga vizuri.
vifaranga hutoka wakati wote na kuzurura hivyo ni hatari kwa wanyama wakali kama vicheche, mwewe na wengine wanaoweza kuwadhuru vifaranga . Ni vyema kutengeneza banda bora kwa ajili ya kufugia vifaranga kwa uangalifu mzuri kukwepa hasara.
Vyombo kwenye nyumba ya vifaranga.
Ni muhimu kuweka vifaa safi kwenye nyumba ya vifaranga kwa ajili ya kuwalishia na kuwalelea. kipo kitu kinaitwa kitalu hiki ni kwa ajili ya kutunzia vifaranga visitawanyike ndani ya banda. Taa ya chemli, jiko la mkaa pia ni vifaa muhimu vya kulelea vifaranga pindi wawapo wadogo banadani bila kuwa na mama yao.
Chanjo na tiba
Vifaranga vinatakiwa kupewa chanjo kulingana na ratiba ya chanjo inavyotaka pindi tu wanapoanguliwa toka kwenye yai lake. wafugaji wengi hawapendi kufuata utaratibu wa chanjo ndiyo maana wengi huambulia hasara pale magonjwa ya milipuko yanapotokea . Ni vyema kumtumia mtaalamu kwa ajili ya maelekezo jinsi na kupata na kutumia chanjo kwa usahihi ili kukwepa kuingia hasara kwa matumizi mabaya ya dawa.
Unapoona tofauti kwenye kuku wako unashauriwa kutumia dawa mapema na kuwatenga vifaranga wote wenye dalili ya kuumwa ili kukwepa kuwaambukiza vifaranga wengine ndani ya banda lako kama mfugaji.