Kisukari ni kati ya Magonjwa ya kwanza kutambuliwa na kuwekwa kwenye maandishi ya Misri ikieleza kama tatizo la “Kukojoa sana”. Wataalamu wa Kihindi waliuita ‘Mkojo wa Asali’ kwasababu unawavutia wadudu
Miaka ya 1500KK Matabibu waliweza kugundua kiwango cha Sukari kwa kuangalia ladha na harufu ya mkojo wa Mgonjwa. Mkojo ukiwa mtamu basi wanahitimisha mhusika ana Kisukari
Utaratibu wa kupima Kisukari Maabara ulianzishwa mwaka 1841 na Karl Trommer ambaye alitumia sampuli ya mkojo kwa kuiweka kwenye ‘Acid Hydrolysis’
