Subscribe Us

Header Ads

Iran haitaachana na masharti yake katika mazungumzo ya nyuklia

 



Iran imesema kuwa haitaachana na masharti yake katika mazungumzo ya nyuklia na madola yenye nguvu duniani. 


Hii ni baada ya Umoja wa Ulaya kusema kuwa muda umewadia kwa Marekani na Iran kufanya maamuzi ya kisiasa yanayohitajika ili kufikia makubaliano. 


Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema serikali inashiriki mazungumzo ya nyuklia kwa kufuata kanuni na mifumo inayowekwa na Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei ambaye ana kauli ya mwisho katika uamuzi wa Tehran.


Mazungumzo ya miezi 11 ya kuufufua muafaka wa nyuklia wa 2015 ambao uliiondolea Iran vikwazo ili nayo ipunguze shughuli zake za nyuklia yamefikia hatua za mwisho. 


Iran inataka iondolewe vikwazo vyote na inataka hakikisho kutoka kwa Marekani kuwa haitajiondoa kwa mara nyingine katika muafaka huo. Mjumbe mkuu wa Iran, Ali Bagheri Kani alirejea Tehran jana kutoka Vienna kwa ajili ya mashauriano zaidi.