Subscribe Us

Header Ads

Bunge Urusi laidhinisha adhabu kwa wanaolikashifu jeshi



Bunge la Urusi limepiga kura kuunga mkono marekebisho ya sheria ambayo yatawezesha kutozwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka 15 gerezani, kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kuhusu vikosi vya jeshi la nchi hiyo. 


Hatua hiyo inachukuliwa katikati mwa ukandamizaji mkubwa dhidi ya uhuru wa habari nchini Urusi, huku ikulu ya Kremlin ikijaribu kuhakikisha kuwa maelezo yake ya vita nchini Ukraine ndiyo yanaufukia umma wa Urusi. 


Vyombo viwili kati ya vichache huru vilivyosalia nchini Urusi - ambavyo ni kituo maarufu cha redio cha Ekho Mosky na chaneli ya habari za mtandaoni ya Dozhd, zimefunga kazi jana Alhamisi, kutoka na ukandamizaji. 


Sheria hiyo inatoa adhabu hasa kwa taarifa zinazodaiwa kuwa za uongo kuhusu wanajeshi wa Urusi, kudharauliwa kwa jeshi la Urusi na miito ya vikwazo dhidi ya Urusi.