Subscribe Us

Header Ads

Watoto wapoteza maisha katika vita Ukraine



Idadi ya raia waliouawa kwenye uvamizi wa Urusi nchini Ukraine inaongezeka siku hadi siku. Kufikia Jumapili, Kamishna wa haki za binadamu wa Ukraine alieleza kuwa idadi ya vifo vya raia imiefikia 210, wakiwemo watoto kadhaa.


Miongoni mwa waliopiteza maisha ni msichana anayefahamika kwa jina la Polina, ambaye alikuwa katika mwaka wake wa mwisho wa kumaliza shule ya msingi katika mji mkuu Kyiv.


Kwa mujibu wa mamlaka za eneo la Kyiv, yeye na wazazi wake waliuawa na mashambulio ya Urusi katika mtaa mmoja kaskazini magharibi mwa mji mkuu. Kaka na dada wa Polina walipelekwa hospitalini kutokana na kujeruhiwa. Dada yake alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kaka yake alipelekwa katika hospitali ya watoto.


Katika mashambulizi hayo, raia wengine kadhaa waliuawa. Msichana mwenye umri wa miaka saba alifariki katika shambulio lililolenga shule ya awali (chekechea) na watu 10 wa jamii ya wagiriki wa Ukraine waliuawa wakati vijiji vyao vilipoanza kushambuliwa kusini mwa nchi hiyo.