Subscribe Us

Header Ads

Utawala wa kijeshi Myanmar wavishutumu vyombo vya habari ya kimataifa kuripoti matukio ya upendeleo



Serikali ya kijeshi Myanmar imelalamika kuhusu ripoti zinazoegemea upande mmoja au za upendeleo kutoka kwa vyombo vya habari vya kigeni, inavyosema vinaripoti vibaya hali ya matukio nchini humo na kutoa habari za uwongo kutoka kwa watu iliowaita magaidi wanaotaka kuivuruga nchi. 


Baraza la utawala nchini humo limetoa taarifa na kusema ni rafiki kwa vyombo vya habari na ulimwengu wa kimataifa, lakini pande hizo mbili zinaharibu juhudi zake za kuhakikisha raia wa Myanmar wanalindwa na pia amani inakuwepo katika nchi hiyo. 


Wizara ya habari imesema inasikitisha kuwa matukio yanaripotiwa bila kuthibitishwa na vyombo hivyo vinavyotoa taarifa kutoka kwa makundi hayo iliyoyaita ya kigaidi. 


Myanmar imekuwa katika mgogoro tangu kufanyika mapinduzi ya kijeshi Februari mosi mwaka jana, yaliyosababisha mauaji ya takriban watu 1,500 yakidaiwa kufanywa na maafisa wa usalama, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wanaharakati walionukuliwa na Umoja wa Mataifa.