Subscribe Us

Header Ads

Ufaransa yasema ni muhimu kukamilisha mazungumzo ya nyuklia ya Iran wiki hii



Ufaransa imesema ni muhimu kwamba wajumbe wa majadiliano ya kujaribu kufufua makubaliano ya 2015 kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wanafikia muafaka wiki hii. 


Pande zote zimeashiria kupiga hatua katika mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Vienna, lakini Iran imesema mataifa ya magharibi bado yanahitaji kuamua juu ya baadhi ya masuala muhimu. 


Mkuu wa ujumbe wa Iran kwenye mazungumzo hayo Ali Bagheri amerejea mjini Vienna baada ya kwenda nyumbani siku ya Jumatano kwa ajili ya mashauriano, na kuacha mazungumzo yakiendelea kwa ngazi ya watalaamu. 


Pande zilizosaini makubaliano hayo ziliyaona kama njia bora zaidi ya kuizuwia Iran kuunda bomu la nyuklia, lengo ambalo Tehran imelikanusha mara zote. 


Wakati wa mazungumzo ya Vienna, Iran imerudia mara kwa mara, wito wa kupewa hakikisho kutoka utawala wa rais Joe Biden wa Marekani, kwamba hakutakuwa na marudio ya kujitoa kama ulivyofanya utawala wa DonaldTrump.