Subscribe Us

Header Ads

Taliban yapiga marufuku waafghanistan kuondoka nchini



Watawala wa Taliban nchini Afghanistan wamewazuia raia wa taifa hilo kuondoka nchini humo, huku maafisa wa kundi hilo wakiendelea kwenda nyumba hadi nyumba mjini Kabul kusimamisha zoezi hilo.


Marufuku ya kusafiri ilitangazwa jana Jumapili na msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid aliyesema zuio hilo linalenga kuwaepusha waafghani na ugumu wa maisha nje ya nchi. 


Juhudi za kuwaondoa Waafghani nchini mwao zinazofanywa na mataifa mbali mbali na mashirika yasio ya kiserikali zimepigwa marufuku na hata familia zinazojaribu kuondoka Afghanistan kwa juhudi zao wenyewe, sasa zinahitaji sababu maalum ya kufanya hivyo la sivyo zitazuiwa na maafisa wa uhamiaji. Wanawake pia wamezuiwa kusafiri isipokuwa wale wanaoandamana na jamaa zao wa kiume.