Subscribe Us

Header Ads

Kremlin yasema ni hatari kwa Umoja wa Ulaya kuipa silaha Ukraine



Urusi imeutuhumu Umoja wa Ulaya kwa mtazamo wa uhasama dhidi yake, ikisema hatua ya kupeleka silaha Ukraine ni hatari na inaendelea kuyumbisha utangamano, na kuwa inadhihirisha kwamba Urusi ilikuwa sahihi kutaka kulivunja jeshi la jirani yake, Ukraine. 


Nchi za Magharibi zimeimarisha mchakato wa kuipa silaha Ukraine ili kuisadia kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi ambao Moscow inauita operesheni maalum ya kijeshi inayonuia kulinda raia wake. 


Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amekataa kuzungumzia idadi kamili ya vifo na majeruhi upande wa wanajeshi wa Urusi au hata kutoa maelezo juu ya hatua ya rais Vladimir Putin kuweka vikosi vyake vinavyoshughulikia masuala ya nyuklia katika tahadhari ya juu.