Serikali imeanza mchakato wa kulipa fidia takribani shilingi million 700 kwa wananchi 411 wa kijiji cha Kidahwe Wilaya ya Kigoma mara baada ya kutoa eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kituo cha kupozea mitambo ya umeme wa Gridi ya Taifa kutokea Nyakanazi mkoani Kagera.
Waziri wa Nishati Dkt. Medad Kalemani amezindua zoezi hilo ambalo limesubiriwa kwa takribani miaka 3 tangu eneo hilo kuchukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarijiwa kuanza kujengwa hivi karibuni.