Subscribe Us

Header Ads

Rais Andrzej Duda aongoza uchaguzi wa Urais Poland


Rais wa sasa wa Poland, mhafidhina Andrzej Duda ameongoza katika uchanguzi wa rais uliofanyika jana nchini humo, lakini atalaazimika kuingia katika duru ya pili kuchuana na meya mliberali wa Warsaw mwezi ujao.

 Kulingana na matokeo rasmi, Duda ambaye anaungwa mkono na chama tawala cha Sheria na Haki (PiS), alikuwa na asilimia 45.24 baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 87 ya kura, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Mshindi wa pili Rafal Trzaskowski kutoka chama cha Jukwaa la Kiraia PO, alikuwa na asilimia 28.92, na hivyo kufaulu kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi utakaofanyika Julai 12.

Mgombea binafsi Rafal Holownia alishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 13.69, huku wagombea wengine wanane wakishindwa kufikisha asilimia 10.

 Kampeni za uchaguzi huo ziligubikwa na wasiwasi kuhusu mmomonyoko wa haki za kidemokrasia pamoja na masuala ya kiuchumi.