Subscribe Us

Header Ads

Lissu amjibu Rais Magufuli asema vita ya Corona haipiganiwi kwa kutumia jeshi la polisi





Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki ( Chadema), Tundu Lissu amemjibu Rais John Magufuli huku akimuambia vita ya Corona haipiganiwi kwa kutumia jeshi la polisi.
Jana Rais Magufuli alikuwa na mkutano na vyombo vya usalama kuhusiana na hali ya ugonjwa wa Corona.
Baada ya mkutano huo Rais alitoa taarifa ya msimamo wa serikali kuwa haitafungia wananchi nyumbani wala kulifunga jiji la Dar es Salaam.
Lissu alisema Corona inapiganiwa kwa kutumia mbinu zinazoshauriwa na wataalamu.
“Zuia mikusanyiko yote. Pima watu, sema ukweli juu ya tatizo, toka mafichoni Chato. Ongoza nchi,” aliandika Lissu katika ukurasa wake wa Twitter.