Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa ombi jipya la kutaka ahutubie wakuu wa mataifa ya Muungano wa Afrika (AU), kulingana na Kamishna wa AU, Moussa Faki.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Bw Faki alisema alipokea ombi wakati wa mazungumzo ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine.
Wawili hao walizungumza kuhusu Rais Zelensky "kutaka kuendeleza uhusiano wa karibu na AU".
Bw Faki hakufichua iwapo ombi hilo litakubaliwa lakini akatuma ujumbe wa twitter kwamba "alisisitizia juu ya haja ya upatikaji wa suluhu ya amani kwa mzozo wa Ukraine".