Subscribe Us

Header Ads

Korea Kusini yawakamata watu wawili kwa kutoboa siri za kijeshi kwa Korea Kaskazini



Korea Kusini imewakamata watu wawili wanaoshukiwa kupeleka siri za kijeshi kwa mtu anayeaminiwa kuwa ni jasusi wa Korea Kaskazini .


Mtendaji mkuu wa ubadilishanaji wa pesa za kidigitali na afisa wa kijeshi alitoa maelezo ya nywila za kufungua taarifa za uongozi wa jeshi wa Korea Kusini.


Polisi wanashutumiwa kwa kupokea kiasi kikubwa cha pesa kwa kufanya hivyo.


Korea Kaskazini na Kusini zimekuwa katika mahusiano ya kutoaminiana tangu zipigane vita kati ya mwaka 1950 na 1953.


"Hiki ni kisa cha kwanza ambapo mwanajeshi aliye kazini na raia kupitia maagizo ya wakala wa Korea Kaskazini walifanya njama na kuilifanyia ujasusi siri za kijeshi kilichogunduliwa’’, imesema polisi.


Saa yenye kamera na kifaa cha USB vilitumiwa kumuwezesha jasusi wa Korea kaskazini kuzifikia data kati ya miezi ya Januari na Machi.


Wanaume hao wawili walikamatwa mapema mwezi huu. Walikopelekwa na utambulisho wa wakala wa Korea kaskazini haijulikani.